🚨TETESI
Klabu ya Young Africans S.C. inatajwa kujiandaa kutuma ofa ya dola 600,000, sawa na zaidi ya bilioni 1.5 za Kitanzania, kwa Al Hilal Omdurman kwa ajili ya kuipata saini ya Jean-Claude Girumugisha 🇧🇮
Girumugisha alisaini mkataba wa miaka sita mwaka 2023 kuitumikia Al Hilal hadi 2029 akitokea Mag Young Boys SC.
Kwa mujibu wa Transfermarkt, thamani yake ya mwisho sokoni ilikuwa euro 75,000, sawa na zaidi ya milioni 229 za Kitanzania, lakini kutokana na kiwango chake msimu huu hasa kwenye michuano ya CAF Champions League, wengi wanaamini thamani yake inaweza kupanda zaidi kabla ya msimu kuisha.
Takwimu zake CAFCL 2025/26:
• Mechi 10
• Magoli 2
• Assist 2
• Kadi za njano 0
• Kadi nyekundu 0
Girumugisha anatajwa kuwa miongoni mwa vijana wenye umri mdogo wanaotarajiwa kufanya makubwa kwenye soka la Burundi na Afrika kwa ujumla.



Post a Comment