SIMBA IMEKUBALI KUMUACHIA CAMARA

 Klabu ya Simba imefikia makubaliano ya kuachana na mlinda mlango wake, Moussa PinPin Camara (27), kuelekea msimu mpya wa ligi wa 2026/27. Uamuzi huo umekuja huku uongozi wa klabu hiyo ukiamua kuendelea kumpa imani mlinda mlango namba moja kwa sasa, Gibrilar Kassali, ambaye amekuwa na kiwango bora langoni. 


Camara, ambaye aliondolewa kwenye mfumo wa wachezaji wa klabu hiyo wakati wa dirisha dogo la usajili kufuatia majeraha makali aliyoyapata kwenye michuano ya kimataifa mwanzoni mwa mwaka huu, tayari amearifiwa kuwa hatatunukiwa mkataba mpya na hivyo yuko huru kutafuta changamoto nyingine.


​Kuondoka kwa mlinda mlango huyo kunahitimisha safari yake ya miaka miwili pekee ndani ya klabu ya Simba tangu alipojiunga nayo. Ikumbukwe kuwa licha ya changamoto za majeraha zilizomuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu, klabu ya Simba ilisimamia na kugharamia matibabu yake yote hadi kuhakikisha amepona kikamilifu na kurejea katika hali yake ya kawaida. #moinfossports #yangascbingwaupdates #simbasctanzania #NBCPremierLeague



0/Post a Comment/Comments