SAMATTA AMECHEKA NA NYAVU

 Nahodha na mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta, amefanikiwa kufungua ukurasa wake wa mabao katika Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1) akiwa na klabu yake ya Le Havre msimu huu wa 2025/2026. Samatta alifunga bao hilo muhimu katika dakika ya 41 wakati wa mchezo uliomalizika kwa sare ya 1-1 dhidi ya OGC Nice, hatua inayozua matumaini mapya kwa staa huyo ambaye amekuwa akipambana kurejesha makali yake ya ufungaji kwenye anga za kimataifa.



​Licha ya kufunga bao hilo Jana Aprili 12, 2026, safari ya mshambuliaji huyo nchini Ufaransa imekuwa na changamoto baada ya kupitia ukame wa mabao katika michezo 19 ya kwanza aliyocheza msimu huu. Kwa mujibu wa ripoti kutoka Ufaransa, bao hili ni muhimu sana kwa ujasiri wa nahodha huyo wa Taifa Stars, huku mashabiki wa soka nchini Tanzania wakimpongeza kwa kuendelea kuiwakilisha nchi vyema na kupambana katika moja ya ligi ngumu zaidi barani Ulaya. #moinfossports #yangascbingwaupdates #simbasctanzania #NBCPremierLeague



0/Post a Comment/Comments