MENEJA wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC, Ahmed Ally amesema kuwa kuelekea mchezo wao wa CAF Champions League dhidi ya Petro de Luanda watakosa huduma ya kipa namba moja Mousa Camara.
Jumapili, wawakilishi wa Tanzania katika anga la kimataifa watarusha karata ya kwanza kwenye hatua ya makundi ikiwa ni msako wa tiketi ya kutinga hatua ya robo fainali.
Ahmed Aly amesema kuwa “Kuhusu mchezo wa Ligi ya Mabingwa Aftika na tunathibitisha utachezwa Novemba 23, 2025 saa 10:00 jioni. Awali walipanga tucheze Novemba 22, 2025 saa 1:00 usiku lakini huo sio muda wetu mzuri wa mauaji hivyo tukafanya jitihada za kubadili muda.
“Mchezo wa Jumapili tutamkosa Moussa Camara ambaye yupo nchini Morocco alipokwenda kufanyiwa matibabu lakini pia tutamkosa beki wetu Abdulrazack Hamza ambaye na yeye anasafiri kwenda Morocco kwa matibabu zaidi. Taarifa njema ni kuwa Mohamed Bajaber amepona na hata mchezo wa kirafiki dhidi ya JKT Tanzania alianza na kucheza dakika 30.
"Viingilio vya mchezo ni Tanzanite - Tsh. 250,000, Platinum - Tsh. 150,000, VIP A - Tsh. 30,000, VIP B - Tsh. 20,000, VIP C - Tsh. 10,000 na Mzunguko - Tsh. 5,000,".
Post a Comment