Petro de Luanda yaichapa goli 1-0 Simba SC CAF Champions League

 


Simba SC 0-1 Petro de Luanda Novemba 23,2025 funga kazi kwa mechi za hatua ya makundi 2025/26. Goli la ushindi limefungwa na Bernardo Dias dakika ya 78. Pasi ya goli hilo pekee la ushindi imetoka kwa Tiago Reis.


Simba SC ikiwa nyumbani rekodi zinaonyesha kuwa ilimiliki mpira asilimia 56 na wapinzani ni asilimia 44. Jumla mashuti 11 Simba SC ilipiga ni moja lililenga lango huku Petro de Luanda wakipiga mashuti 7 na katika hayo mawili yalilenga lango.

Wageni Petro de Luanda wanaongoza kundi D kwenye msimamo wakiwa na pointi tatu muhimu huku mnyama Simba SC akiburuza mkia akiwa hajakusanya pointi.

Zimeshuhudiwa dakika 90 bila pigo la kona mchezo wa leo. Petro de Luanda mbinu kubwa ilikuwa ni kushambulia kwa kushtukiza huku Simba SC wakijilinda hasa kipindi cha kwanza ambapo walianza bila mshambuliaji halisia.

Mchezo wa leo kikosi cha kwanza cha Simba SC kilianza bila uwepo wa mshambuliaji halisia ambapo Joshua Mutale alikuwa kwenye eneo hilo yeye ni kiungo mshambuliaji.

0/Post a Comment/Comments