CAF Champions League leo Novemba 22,2025 ubao wa Uwanja wa New Amaan Complex umesoma Yanga SC 1-0 AS FAR Rabat mchezo wa hatua ya makundi.
Goli la ushindi limefungwa na mshambuliaji Prince Dube ambaye alianza kikosi cha kwanza. Ni dakika ya 58 Dube alipachika bao hilo kwa pasi ya kiungo Mudathir Yahya.
Kampeni za hatua ya robo fainali zimeanza huku Yanga SC kete ya kwanza wakikomba pointi tatu kundi B.
Msimamo upo namna hii:-
1. Yanga SC pointi 3 mechi 1
2. JS Kabylie pointi 0 mechi 0
3. Al Ahly pointi 0 mechi 0
4. AS FAR Rabat pointi 0 mechi 1
Yanga SC chini ya Kocha Mkuu, Pedro Goncalves imeanza kwa ushindi ikiwa ni mchezo wa kwanza wakiwa nyumbani katika hatua ya makundi.
Kabla ya mchezo mshambuliaji wa Yanga Clement Mzize aliwashukuru mashabiki kwa kumpigia na kutwaa tuzo ya goli bora la CAF 3035.
.jpg)
Post a Comment