Yanga SC yatinga hatua ya makundi Afrika


WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga SC wametinga hatua ya makundi kwa kuwaondoa Silver Strikers ya Malawi.

Kwenye mchezo uliochezwa Oktoba 25,2025 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga SC 2-0 Silver Strikers CAF Champions League.

Matokeo ya ushindi yameifanya Yanga SC kuandika rekodi ya kufuzu hatua ya makundi kwa msimu wa 2025/26 baada ya ule wa ugenini Oktoba 18,2025 kupoteza kwa kufungwa bao 1-0.

 Yanga SC ilifunga mabao yote mawili kipindi cha kwanza yalitosha kuwapa tiketi wawakilishi wa Tanzania kusonga mbele mpaka hatua ya makundi Afrika.

Ni Dickson Job alifungua pazia la kufunga dakika ya 6 kwa asisti ya Doumbia ambaye alipiga kona baada ya Duke Abuya kufanya jaribio akiwa nje kidogo ya 18.

Kiungo Pacome alifunga bao la pili dakika ya 34 likitosha kuipeleka Yanga SC hatua ya makundi kwa msimu mpya wa 2025/26.

Yanga SC inatinga hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla ya mabao 2-1 Silver Strikers ambao walikuwa wanaamini wamemaliza mchezo.

0/Post a Comment/Comments