Yanga SC hesabu zao ndefu CAF Champions League

 


Walter Harson, Meneja wa Yanga SC ameweka wazi wataandika historia Jumamosi kwa kutinga hatua ya makundi licha ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Silvers Strikers.

Ipo wazi kwamba Oktoba 18, 2025 matokeo yalikuwa Silver Strikers 1-0 Yanga SC CAF Champions League mchezo uliochezwa Uwanja wa Bingu.

 Goli la ushindi lilifungwa dakika ya 76 na Andulu Yosefe na mchezo mmoja wa maamuzi utachezwa Uwanja wa Mkapa, Oktoba 25, 2025..


Walter amesema: “Hii ni Champions League tunakwenda kuandika historia kwenye mchezo wa Jumamosi ambapo tunaamini kwamba tutafanya vizuri na kutinga hatua ya makundi.

“Mashabiki watambue kwamba matokeo ya mchezo uliopita hayo yamekwisha hivyo kwa sasa tunafanya maandalizi kwa mchezo wetu ujao, wajitokeze kwa wingi Uwanja wa Mkapa kwa kuwa maandalizi yameanza,".

0/Post a Comment/Comments