Yanga SC 2-0 Mtibwa Sugar, Zimbwe Jr atwaa tuzo


Yanga SC imepata ushindi wa mabao 2-0 Mtibwa Sugar NBC Premier League leo Uwanja wa KMC Complex.

Mchezo huo ulianza kuchezwa  saa 10:00 jioni kwa wababe hao wawili kuvuja jasho kusaka pointi tatu Oktoba 28,2025. 

Mabingwa watetezi Yanga SC wamebeba pointi tatu huku beki Mohamed Hussen Zimbwe Jr akichaguliwa kuwa mchezaji bora.

Zimbwe Jr alifunga bao hilo akiwa nje ya 18 kwa shuti kali akiwa nje ya 18 kwa mguu wake wa kushoto.

Bao la pili lilifungwa na Celstin Ecua dakika ya 83 kwa shuti kali akiwa nje ya 18 kwa mguu wa kushoto akitumia pasi ya Maxi Nzengeli.

0/Post a Comment/Comments