Simba SC imetinga hatua ya makundi kwa kuwaondoa Nsingizini Hotspurs kwenye CAF Champions League.
Timu hiyo kutoka Tanzania kwenye mchezo wa pili ilikwama kufunga wala kuruhusu goli la kufungwa.
Ilikuwa ni mechi ya Jumapili Oktoba 26,2025 iliamua nani atakata tiketi kutinga hatua ya makundi Afrika.
Kwenye mchezo wa kwanza ugenini ilikuwa Nsingizini Hotspurs 0- 3 Simba SC, Oktoba 19,2025. Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mabao ya Simba SC yalifungwa na Wilson Nangu na Kibu Dennis alifunga jumla ya magoli mawili kwenye mchezo huo.
Katika mchezo wa Uwanja wa Mkapa, Kibu Dennis alianza kikosi cha kwanza na kuvaa kitambaa cha unahodha.
Simba SC inaungana na Yanga SC kwenye timu kutoka Tanzania ambazo zimetinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.

Post a Comment