Simba SC yagomea matokeo ya CAF Champions League ugenini


UONGOZI wa Simba SC umegomea matokeo waliyopata ugenini kwenye mchezo wa CAF Champions League dhidi ya Nsingizini Hotspurs Oktoba 19,2025 kwa ubao kusoma Nsingizini Hotspurs 0-3 Simba SC.

 Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC, Ahmed Ally ameweka wazi kuwa matokeo waliyopata ugenini wanayaacha hukohuko ikiwa ni zawadi kwa mashabiki wa Eswatini wana kazi nyingine yakufanya Uwanja wa Mkapa.

Baada ya ushindi wakiwa ugenini kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Somholo, mchezo wa pili unatarajiwa kuchezwa Oktoba 26,2025 Uwanja wa Mkapa ambao utatoa mshindi wa jumla atakayetinga hatua ya makundi.

Ahmed amesema: “Tumepata ushindi wa mabao 3-0 ugenini haya matokeo ni zawadi kwa mashabiki wa Eswatini bado sisi tunakwenda kuanza upya Uwanja wa Mkapa. Yaani tutaingia uwanjani kama hatujafunga vile kwa kuwa kazi inaanza upya,".

 Simba SC walifanikiwa kutengeneza nafasi nyingi zaidi. Bao la kwanza la mchezo huo lilikuja dakika ya 45 ya mchezo, kupitia kwa mlinzi wa Simba SC, Wilson Nangu.

Mara baada ya majaribio kadhaa Simba SC walifanikiwa kupata bao la pili kupitia kwa, Kibu Dennis dakika ya 82 kamba ya tatu ilifungwa na Kibu dakika ya 89.

0/Post a Comment/Comments