Simba SC kuondoka na kijiji cha watu 50 kuelekea Eswatin


MSAFARA wa Simba SC unatarajiwa kuondoka Dar Oktoba 16 2025 kuelekea nchini Eswatini kwa maandalizi ya mwisho ya mchezo wa raundi ya kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Nsingizini Hotspurs.

Ni kijiji cha watu 50 kinatarajiwa kuwa katika msafara huo ukijumuisha wachezaji 22, benchi la ufundi likiwa na kijiji cha watu 12 wengine wakiwa ni maofia na viongozi wa Klabu ya Simba SC.

Ikumbukwe kwamba Oktoba 19,2025 mchezo huo unatarajiwa kuchezwa na ule wa marudinao unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Oktoba 24,2025 na utaamua mshindi wa jumla atakayetinga hatua ya makundi.

Kwa sasa kikosi kipo kambini Mbweni ikiwa ni maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo huo ambao utakuwa ni wa kwanza kwa Meneja Mkuu, Dimitar Patev aliyekuwa anakifundisha kikosi cha Gaborone United.

Meneja huyo amekuja kuchukua mikoba ya Fadlu Davids ambaye kwa sasa yupo kwenye changamoto mpya katika Klabu ya Raja Casablanca ya Morocco.

Simba SC ilitinga hatua inayofuata kwa kuwafungashia virago Gaborone kwa ushindi wa jumla ya magoli 2-1 ilipata ushindi wa 1-0 ugenini na mchezo wa pili uliochezwa Uwanja wa Mkapa ilikuwa 1-1.

0/Post a Comment/Comments