Romain Folz Kocha Mkuu wa Yanga SC amebainisha matarajio kimataifa

 


ROMAIN Folz, Kocha Mkuu wa Yanga SC amebainisha kuwa matarajio yao kwenye anga la kimataifa ni kupata matokeo mazuri kwenye mchezo ujao dhidi ya Silver Strikers ya Malawi.

Yanga SC inatarajiwa kushuka uwanjani Oktoba 18,2025, msafara wa wachezaji 24 umekwea pipa Oktoba 16 kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kuelekea kwenye mchezo huo.

Folz amesema: “Yapo matarajio ambayo tunayo lakini ni muhimu kuona kwamba tunafikia malengo ya mwisho. Kinachohitajika ni matokeo na hicho kinatazamwa. Hakuna tofauti kubwa kwenye kile ambacho tunakifanya.

“Kikubwa ni kwamba tunamuheshimu mpinzani wetu na malengo makubwa ni kuona kwamba tunapata matokeo mazuri kwenye mchezo wetu. Tunajitahidi kuona kwamba tunakuwa imara katika kila Idara. Unajua unaona kuna mabadiliko ambayo yapo.

“Muda wote ninasema kwamba kuna mabadiliko na namna ambavyo inakuwa hivyo ni kutokana na mchakato ambao tunaufanya.

“Ninarudia kwa wakati mwingine mara kwa mara. Kile ambacho tunafanya ni kwa ajili ya mashabiki. Ikiwa hatutakuwa tunafanya vizuri ni jambo ambalo hatufurahii. Yote ni kwa ajili ya mashabiki na tunaendelea kuona kwamba wanakuwa na furaha. Tunafurahi kuona wapo nasi kila hatua kwa hatua hilo ni jambo kubwa. Tutapambana kufanya vizuri hapo kwa ajili yao,".

0/Post a Comment/Comments