Mara baada ya kipigo cha goli 1-0 katika mchezo wa CAF Champions League walichopokea Yanga SC dhidi ya Silver Strikers, Romain Folz amevunjiwa mkataba wake jumlajumla.
Folz alikuwa Kocha Mkuu wa Yanga SC kwenye mwanzo wa msimu, kwa sasa hatakuwa kwenye benchi l ufundi huku mchakato wa kumtafuta kocha mpya ukiendelea.
Taarifa kutoka Yanga SC liyotolewa Oktoba 18 2025 inaeleza namna hii:-
“Uongozi wa Young African Sports Club unapenda kuutarifu Umma kuwa, umevunja mkataba na Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza, Romain Folz.
“Uongozi wa Young African Sports Club unamshukuru kocha Romain Folz kwa mchango wake ndani ya klabu yetu na unamtakia kila la kheri katika majukumu yake yanayofata.
“Katika kipindi hiki kikosi chetu kitakuwa chini ya kocha msaidizi Patrick Mabedi huku mchakato wa kutafuta kocha mkuu ukiendelea,” ilieleza taarifa hiyo.

Post a Comment