NGOMA ni nzito kuelekea mchezo ujao wa kimataifa kwa wawakilishi wa Tanzania Yanga SC kutokana na aina ya wapinzani ambao watakutana nao.
Yanga SC chini ya Kocha Mkuu Romain Folz inasaka hatua ya kutinga hatua ya makundi kwenye anga la kimataifa kikwazo kilichopo mbele yao ni mchezo wa kwanza ugenini mbele ya timu yenye rekodi nzuri kwenye mechi za nyumbani.
Ikumbukwe kwamba kituo kinachofuata katika CAF Champions League, Silver Strikers vs Yanga SC Oktoba 18, 2025 Uwanja wa Bingu,Malawi.
Silver Strikers katika mechi 20 zilizopita walipata ushindi kwenye mechi 10 na wamekuwa na rekodi nzuri kwa mechi za nyumbani katika mechi 6 walishinda 3 hivyo wapinzani hawa sio wanyonge.
Upande wa Yanga SC katika mechi 6 zilizopita ni ushindi katika mechi 5 huku wakiwa na rekodi nzuri mashindano ya kimataifa.
Katika Ligi ya Malawi Silver Strikers ipo nafasi ya tatu inakutana na Yanga SC ambayo katika ligi ya NBC ipo nafasi ya nne kwenye msimamo.
Tayari msafara wa Yanga SC umewasili salama Malawi kwa mchezo huo muhimu huku mshambuliaji Clement Mzize, Dickson Job, Zimbwe Jr wakiwa miongoni mwa wachezaji waliopo Malawi.

Post a Comment