Na Andrew Chale
MBUNIFU
na mwanamitindo (model) Rodrick Charles maarufu kwa jina la ‘Rodney de
lativo’ amefariki dunia leo (Mei 30) baada ya kuugua kwa muda alipokuwa
amelazwa Hospitali ya Jeshi, Lugalo.
Akizungumza
na Mtandao huu mapema leo kwa njia ya simu, Rafiki wa karibu wa
familia ya marehemu, David Msangi alisema marehemu alipatwa na umauti
alipokuwa akiendelea na matibabu katika Hospitali ya Lugalo, alipokuwa
amelazwa na msiba huo hupo nyumbani kwa marehemu Tabata Bonyokwa.
“Tumempoteza
mtu muhimu sana ambaye alikuwa na mawazo mengi ya kufikia mafanikio
yake. Tutaendelea kumkumbuka.” Alisema Msangi ambaye pia alikuwa
mshahuri wa karibu wa marehemu.
Msangi
alisema kwa mujibu wa familia ya marehemu, anatarajiwa kuzikwa hiyo
Jumamosi Mei 31huko huko kwenye makaburi ya Tabata Segerea.
Wakati
wa uhai wake, marehemu alifanya kazi kwenye majukwaa mbalimbali na
wabunifu na wanamitindo wakubwa wakiwemo wabunifu Ally Remtullah,
Mustapha Hassanali, Asia Idarous. Wanamitindo Rio Poul, Martin Kadinda,
Justine, Faustine Simon na wengine wengi.
Rodney mpaka anakutwa na umauti, alikuwa mshahuri na model wa kampuni ya Crisswelly African Fashion.
Mareehemu
alizaliwa Mei 26, 1994. Elimu yake alisomea Magoze Sekondari na
kuhitimu 2011 na kuingia moja kwa moja kwenye fani ya uwanamitindo na
kuendelea hadi alipokutwa na umauti.
Aidha,
kwa jamaa wa karibu na wabunifu na wanamitindo kwa watakaotaka maelezo
ya kufika kwa marehemu wanaweza kuwasiliana na David Msangi kwa namba
hii 0652901684
..Rest In Peace Rodney. Daima utakumbukwa!